Uchanganuzi linganishi wa usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya ya Kiswahili

Show simple item record

dc.contributor.author Kimondiu, Dorcas K.
dc.contributor.author Musyoka, Francis
dc.contributor.author Chomba, Esther N.
dc.date.accessioned 2026-09-23T08:13:56Z
dc.date.available 2026-09-23T08:13:56Z
dc.date.issued 2025
dc.identifier.citation European journal of linguistics, volume 4, issue No. 2, pp 49-67, 2025 en_US
dc.identifier.issn 2957-4641
dc.identifier.uri https://carijournals.org/journals/ejl/article/view/2936/4350
dc.identifier.uri https://repository.seku.ac.ke/handle/123456789/8440
dc.description.abstract Makala haya yanakusudia kuchanganua na kulinganisha wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili ambazo ni: Mwisho wa Kosa,(1987) iliyoandikwa na Zainabu Burhani, Siku Njema(1996), iliyoandikwa na Ken Walibora, Taswira za Mawingu, (2011) iliyoandikwa na Sinjiri Mukuba na Nguu zaJadi,(2021) iliyoandikwa na Clara Momanyi. Makala haya yanaegemea nadharia ya Mwanamume Mpya. Nadharia hii iliasisiwa na Beynon (2002). Nadharia ya Mwanamume Mpya inajaribu kueleza kwa nini baadhi ya wanaume hukaa na wake zao kwa usawa bila kuonesha tabia za mfumo dume ambazo huashiria kuwepo kwa taasubi ya kiume. Mihimili ya nadharia ya Mwanamume Mpya iliyoongoza makala haya ni kusaidia wake zao na wanawake wengine katika jamii kujiendeleza kielimu na kikazi, kukubali majukumu yoyote ya kiuana bila kujali jinsia au watu wanaomzunguka, kutoonesha udikteta katika familia zao pamoja na jamii inayowazunguka, kuwaona wanawake kama viumbe sawa na wanaume kwa kuwaheshimu na kuwapenda katika kila nyanja wanazokuwepo na kukosoa nafsi zao na mazoea yao kama wanaume. Mbinu ya Fasihi Linganishi imetumika kulinganisha na kulinganua usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya teule. Data iliyotumika katika Makala haya ilitolewa maktabani. Maktabani, tasnifu, makala na vitabu vinavyohusiana na mada vilisomwa kwa kina. Uwasilishaji wa matokeo umefanyika kwa njia ya maelezo na michoro faafu. Matokeo yameonesha kuwa waandishi wa kike wamemsawiri mwanamume kwa mtazamo chanya ikilinganishwa na waandishi wa kiume. Kwa hivyo, kulingana na waandishi wa kike mwanamume ni mpya. Kulingana na mpito wa wakati waandishi wa karne ya ishirini wamemsawiri mhusika wa kiume kwa mitazamo chanya ikilinganishwa na waandishi wa karne ya ishirini na moja. Kwa hivyo mwanamume ni mpya kulingana na waandishi wa karne ya ishirini. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.subject usawiri en_US
dc.subject wahusika en_US
dc.subject uchanganuzu en_US
dc.subject ulinganishi en_US
dc.subject mtazamo en_US
dc.title Uchanganuzi linganishi wa usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya ya Kiswahili en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search Dspace


Browse

My Account