Abstract:
Kusudi: Utafiti  huu  ulichunguza  usahihi  wa  uhawilishaji  wa  viwakilishi  vya  jinsia  katika vitabu  vya  Kiingereza  vilivyotafsiriwa  kutoka  Kiswahili  kwenda  Kiingereza. Utafiti huu ulidhamiria kuchunguza na kubainisha usahihiwa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia kutoka kiswahili  lugha  isiyo  na  viwakilishi  bainifu  vya  jinsia  kwenda  kiingereza  lugha  yenye viwakilishi bainifu ya jinsia.  Mbinu: Data  za  utafiti  zilipatikana  kwa  kusoma,  kuchanganua  na  kuhakiki  tafsiri  ya  vitabu teule vya fasihi: Siku Njemaya Walibora (1996) na tafsiri yake A Good Dayiliyotafsiriwa na Kweyu na Kawegere (2019), Kaburi bila Msalabailiyoandikwa na Kareithi (1969) na tafsiri yake  ya  Kiingereza Unmarked  Graveiliyotafsiriwa  na  Githiora (2017).  Vilevile,  mtafiti aliangazia tamthilia mbili; Tamthilia ya Natalailiyoandikwa na Mberia (1997) na tafsiri yake ya  Kiingereza Natalailiyotafsiriwa  na  Kasu  na  Marami  (2011).  Tamthilia  ya Kinjekitileiliyoandikwa na Hussein (1969) na tafsiri yake Kinjekitileiliyotafsiriwa na Hussein mwenyewe (1970) ilichunguzwa. Mtafiti aliteua vitabu hivi kwa kuwa vilionesha utajiri wa data inayohusu uhawilishaji  wa  viwakilishi  vya  jinsia. Utafiti  huu  uliongozwa  na  Nadharia  ya Skoposna Nadharia  ya Usawa wa Kidhima. Nadhariaya Skoposiliyoasisiwa na Hanns Vermeer (1978) ambayo husisitiza kuwa, kimsingi kutafsiri kunafaa kushughulikia jukumu la matini chanzi na matini  lengwa  yaani  tafsiri  ni  kitendo  chenye  malengo. Nadharia  ya  Usawa  wa  Kidhima iliasisiwa  na  Nida  (1964)  na  inatilia  mkazo  usawa  wa  kimaana  na  athari  sawa  kwa  hadhira katika  mchakato  wa  tafsiri. Baada  ya  kubainisha  uhawilishaji  wa  viwakilishi  vya  jinsia,  data hiyo  ilichanganuliwa kitaamuli  na  kitakwimu  na matokeo  kuwasilishwa  kupita  maandishi  ya kinadhari majedwali na michoro ya miche duarakutathimini usahihi uhawilishaji huo. Matokeo: Matokeo ya  utafiti huu yanaonesha kuwa wafasiriwa vitabu teule wamehawilisha viwakilishi  vya  jinsia  kwa  usahihi  na  uhawilishaji  mwingine  ukazua  utata.Uhawilishaji  wa viwakilishivya  jinsia  unachangamoto  nyingi  kwa  hivyo  wafasiri  wanapaswa  kumakinika kwani, uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia huwa na athari asi na chanya kwa hadhira lengwa. Mchango wa kipekee kwa nadharia, vitendo na sera:Utafiti huu unapendekeza utafiti zaidikufanywa katika  uhawilishaji  wa  viwakilishi  vya  nyakati  katika  tafsiri  kutoka  Kiswahili kwenda  Kiingereza  kwani  kama  uhawilishaji  wa  viwakilishi  vya  jinsia,  uhawilishaji  wa viwakilishi vya wakati vilevile, vinaweza kuwa na athari kwa ujumbe asilia.