Abstract:
Makala hii imechunguza, usawiri wa wahusika wa kume katika riwaya ya Chozi la Heri(2017). Katika ulimwengu  wa  riwaya  ya  Kiswahili  na  fasihi,  imekuwa  kama  jambo  la  kawaida  kuona watafiti wengi wakichunguza masuala ya wanawake zaidi kuliko masuala ya wanaume. Jambo hili limetokana na ukweli kwamba, wanawake wamekuwa wakipiganiwa haki zao ili kuwafanya sawa na wanaume katika nyanja mbalimbali za maisha. Atieno(2019) anaeleza kuwa, kupuuzwa kwa jinsia ya kiume kumechangia hali yao ya upweke, kwani hakuna anayewafikiria wala kuwatetea kama  inavyofanyiwa  jinsia  ya  kike.  Riwaya  hii  imeteuliwa  kimakusudikwa  sababu  inamsawiri mhusika  wa  kiume  katika  nyanja  mbalimbali za  maisha.  Makala  hii  iliogozwa  na  nadharia  ya uhalisia.Nadharia ya uhalisia inadai kwamba, fasihi inatakiwa kutoa picha halisi ya jamii husika.Nadharia  hii  ilizuka  huko  Ulaya  katika  karne  ya  kumi  na  tisa.Utafiti  huu  ulifanyika  maktabani ambapo riwaya ya Chozi la Heriilisomwa na kuhakikiwa. Ni matumaini yetu kuwa, Makala hii imetoa  mwanga  mkubwa kuhusiana  na  masuala  ya  jinsiaya  kiume.  Aidha, Makala  hii  itakuwa kichocheo cha watafiti wa baadaye wa fasihi kuchunguza masuala yanayohusu jinsia ya kiume