Abstract:
Makala  haya  yameonyeshakwambamatumizi  ya  tafsiri  hususanuteuzi  wa  mikakati  ya  tafsiri katikaufundishaji wa lugha kama nyenzo ya kurahisisha mawasiliano hukabiliwa na changamoto mbalimbali. Data zilikusanywa kupitia ushuhudiaji na uchambuzi wa nyaraka. Kulingana naCook (2018)tafsiri  ni mchakato  unaohusisha  uteuzi  wa  mikakati  ya  tafsiri  ambayo  ndiyo  msingi anaotumia  mfasiri  anapokabiliwa  na  tatizolaukosefu  wa  visawe  vya  moja  kwa  moja  baina  ya lugha  chanzi  (kuanzia  sasa  LC)  na  lugha  lengwa  (kuanzia  sasa,  LL). Tafiti  tanguliziMohamed (2014),Ngwendu (2016), Ito (2017), Mahi (2018), Navidinia na wenzie (2019), Karimah (2020) na Ngesu (2020) kuhusutafsiri na ufundishaji wa lugha ya kigenihazijachunguza changamoto za uteuzi wa mikakati ya tafsiri katikahali halisi darasaniilazimejiegemeza kuchunguza changamoto za  tafsiri  kwa  jumla. Uteuzi  wa  mikakati  ya  tafsiri isiyofaa  unaweza  kukwamisha  mawasiliano katika ufundishaji na unaweza kuwa naathari hasi kwa mwanafunzi anayejifunza lugha. Hivyo, ilionekana  ni  muhimu  kuchunguza  uteuzi  wa  mikakati  ya  tafsiri  katika  mchakato  halisi  wa ufundishaji   wa   Kiswahilidarasani. Matokeo   yanaonesha   kwamba   walimu   na   wanafunzi hukabiliana na changamoto mbalimbali kutokana na kutumia mkakati wa tafsirisisisi kwa lengo la kurahisisha  mawasiliano.  Inapendekezwakuwa walimu  ambao  hawana  maarifa  na  umahiri katika   taaluma   ya   tafsiri   waepuke   kutumia   tafsiri   katika   ufundishaji   wa   Kiswahili.   Pia, inapendekezwa  kuandaawarsha  za  mara  kwa  mara  ili  kuwasaidia  walimu ambao  tayari wamesoma kozi mbalimbali za tafsiri ili kuboresha umahiri wao katika tafsiri. Pia, inapendekezwa kuwawezesha  walimu  na  wanafunzi  kuwa  na  vitendeakazi  kama  vile  kamusi  thaniya  na  kamusi wahidiya.