Abstract:
Kamusi ni kitabu chenye vipengele vya kileksia vinavyopangwa kwa utaratibu fulani au muundo,
kikiwa na taarifa muhimu kuhusu vipashio hivyo (Elkateb, 2014). Miongoni mwa vigezo
vinavyotumiwa kuainisha kamusi ni lugha. Vigezo vingine ni ukubwa, walengwa na maudhui.
Taarifa inayotolewa inaweza kuwa katika lugha moja na kuunda kamusi Wahidiya au katika
lugha mbili (Kamusi Thaniya) au lugha zaidi ya mbili na kuunda Kamusi Mahuluti. Kamusi
thaniya na mahuluti hutumiwa katika mchakato wa tafsiri na pia hujulikana kama kamusi ya
wingilugha. Jamii nyingi ulimwenguni huwa jamii lugha ulumbi ambapo lugha zaidi ya mbili
huzungumzwa. Sura hii inajadili tafsiri tenge kwenye kamusi thaniya ya Kiingereza-Kiswahili
(TUKI, Toleo la Tatu).