Abstract:
Uteuzi wa mikakati ya tafsiri katika mchakato wa tafsiri, ni suala
muhimu katika Nadharia ya Tafsiri. Lengo la makala haya ni kutathmini
mikakati ya tafsiri iliyotumiwa katika kutafsiri ya riwaya ya Kiswahili
Siku Njema iliyotafsiriwa kwenda Kiingereza kama A Good Day. Uteuzi
wa mikakati ya tafsiri unaweza kuwa na athari zake katika uhawilishaji
wa ujumbe. Hata hivyo, suala hili halijapewa nafasi inayostahiki katika
tafiti tangulizi kuhusu kazi za tafsiri. Tathmini za tafsiri hujikita
kuchanganua changamoto za tafsiri bila kuonesha kwamba uteuzi wa
mikakati ya tafsiri una mchango mkubwa katika kuibua changamoto
hizo. Modeli ya Vinay na Derbelnet (2004) ilitumiwa kubaini mikakati
ya tafsiri iliyotumiwa na wafasiri Dorothy Kweyu na Fortunatus
Kawegere. Wataalamu wanakubaliana kwamba Modeli ya Vinay na
Derbelnet ndio msingi wa uainishaji wa mikakati ya tafsiri na wataalamu
wengine wanaoainisha mikakati ya tafsiri hutumia modeli hii kama
msingi wa uainishaji wao.