Please use this identifier to cite or link to this item: https://repository.seku.ac.ke/handle/123456789/5585
Title: Tathmini ya mikakati ya tafsiri ya Vinay na Derbelnet (2004) katika tafsiri ya A Good Day (2019)
Authors: Ngesu, Sarah N.
Malangwa, Pendo S.
Kandagor, Mosol
Keywords: Mikakati ya Tafsiri
Siku Njema
A Good Day
Issue Date: Sep-2019
Citation: Jarida la Mwanga 4(1); 129-152
Abstract: Uteuzi wa mikakati ya tafsiri katika mchakato wa tafsiri, ni suala muhimu katika Nadharia ya Tafsiri. Lengo la makala haya ni kutathmini mikakati ya tafsiri iliyotumiwa katika kutafsiri ya riwaya ya Kiswahili Siku Njema iliyotafsiriwa kwenda Kiingereza kama A Good Day. Uteuzi wa mikakati ya tafsiri unaweza kuwa na athari zake katika uhawilishaji wa ujumbe. Hata hivyo, suala hili halijapewa nafasi inayostahiki katika tafiti tangulizi kuhusu kazi za tafsiri. Tathmini za tafsiri hujikita kuchanganua changamoto za tafsiri bila kuonesha kwamba uteuzi wa mikakati ya tafsiri una mchango mkubwa katika kuibua changamoto hizo. Modeli ya Vinay na Derbelnet (2004) ilitumiwa kubaini mikakati ya tafsiri iliyotumiwa na wafasiri Dorothy Kweyu na Fortunatus Kawegere. Wataalamu wanakubaliana kwamba Modeli ya Vinay na Derbelnet ndio msingi wa uainishaji wa mikakati ya tafsiri na wataalamu wengine wanaoainisha mikakati ya tafsiri hutumia modeli hii kama msingi wa uainishaji wao.
URI: http://repository.seku.ac.ke/handle/123456789/5585
Appears in Collections:School of Humanities and Social Sciences (JA)



Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.