dc.description.abstract |
Makala haya yanachunguza mchakato wa katafsiri kwa Tafsiri- Mashine. Tafsiri- Mashine baina ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza hutumiwa na wasorni, wafasiri, watalii, watafiti na wajifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni au ya pill. Kwa hivyo, ni nyenzo muhimu katika mchakato wa kutafsiri matini. Hata hivyo, mchakato huu unakabiliwa na changamoto za tafsiri tenge kama inavyodhihirika katika makala haya. Mbinu ya uchambuzi wa matiniilitumiwa kukusanya data iliyojenga msingi wa makala haya. Matin! zilizotafsiriwa kwa kutumia Tafsiri- Mashine (kuanzia sasa, TM) zilichanganuliwa kiulinganishi, Matokeo yanaonesha kwamba tafsiri ya neno kwa neno inayotumika kwa upana katika TM ina upungufu katika kuhawilisha maana kutoka Kiingereza (lugha chanzi) kwenda Kiswahili (lugha lengwa). Tafsiri haihusishi tu maneno na sentensi bali ni mchakato changamani unaohusisha vipengele vingi. Mwandishi wa makala haya ameonesha mifano anuwai ya tafsiri tenge na kutoa mapendekezo ya kukabiliana na changamoto hizo. Matokeo ya utaftti huu yamebainisha kwamba lugha nyingi za Kiafrika ikiwemo lugha ya Kiswahili, hazijaweza kufaidi katika mbinu hii ya kutafsiri kwa mashine (kompyuta). |
|