Utathimini wa maudhui katika tamthilia zilizoteuliwa kutahiniwa katika shule za upili nchini Kenya: Mstahiki Meya (2009) na Kigogo (2016).

Show simple item record

dc.contributor.author Muthui, Evelyn Kakivi
dc.contributor.author Chomba, Esther N.
dc.date.accessioned 2019-07-17T07:23:16Z
dc.date.available 2019-07-17T07:23:16Z
dc.date.issued 2019
dc.identifier.citation International journal of advanced research, 6(11), 130-137 en_US
dc.identifier.issn 2320-5407
dc.identifier.uri http://www.journalijar.com/uploads/366_IJAR-25170.pdf
dc.identifier.uri http://repository.seku.ac.ke/handle/123456789/4496
dc.description DOI: 10.21474/IJAR01/7979 en_US
dc.description.abstract Utafiti huu unalenga kutathmini uhalisia wa maudhui katika tamthilia zilizoteuliwa kitahiniwa katika shule za upili hususan tamthilia ya mstahiki meya (Arege, T. 2009) na Kigogo (Kea, P. 2016). Katika kuzisoma tamthilia hizi na kuzitathmini tamthilia hizi, ni kweli kuwa tamthilia hizi zina ukaribiano wa kimaudhui lakini je kazi hizi za tamthilia zilihahakisi uhalisia wa mambo katika jamii kipindi ambacho ziliteuliwa kutahiniwa? Hata hivyo mtafiti alijiuliza kuwa je, ni kigezo kipi kinatumiwa kuteuwa tamthilia hizi kuwa za kutahiniwa katika kipindi Fulani ilhali zafanana kimaudhui? Je ni hali halisi ya kimaisha katika jamii wakati wa kuteua kazi hizi? Ikiwa ni hivyo,mtafit anatarajia kuzichunguza tamthilia hizi ili kubainihali ya uhalisia wa kijamii wakati katika kpindi cha kuteuliwa tamthilia hizi ili kubaini ufaafu wake kwa wanafunzi ambao ni kiwakilishi cha jamii kwa wakati ule.Utafiti huu utatathmini maudhui katika tamthilia hizi na kuonyesha umuhimu wake kwa wanafunzi na uhalisia wake katika jamii katika kipindi cha kuteuliwa kwake.Tutauchanganua maudhui katika kazi hizi mbili mintaaarafu matukio na hali halisi za kijamii na kuzitathmini tukitumia nadharia ya uhalisia. Kwa kutumia msingi ya nadharia ya Uhalisia ili kufikia maamuzi ya kuwa ama maudhui ya tamthilia hizi yalifaa kwa kipindi cha kuteuliwa au la. Mtafiti atapendekeza njia mwafaka za kuteua kazi za fasihi za kutahiniwa kwa kurejelea matokeo ya utafiti wetu.Ili kufikia malengo yetu, utafiti utazichanganua tamthilia hizi kwa undani na tutarejelea matukio halisi kama yalivyoripotiwa katika vyombo vya habari, kusakura kwenye mitandao kubaini masuala halisi jamii kama vile ; maudhui ya kisiasa, mungawanyiko wa jamii kwa mipaka ya kijamii, chuki, ukabila miongoni mwa mambo mengine yanayoiadhiri jamii ya leo na kisha kutathmini kwa kutumia nadharia teule ya uhalisia ili kubaini iwapo tamthilia ambazo zinateuliwa zinalenga mambo yale kwa kuangalia maudhui makuu ya tamthilia ya Mstahiki Meya(2009)na Kigogo(2016).Ni bayana kwamba mengi ya kuhusu maudhui yamefanywa katika tamthilia hizi hasa ikichukuliwa kwamba ni kazi ambazo zimetahiniwa katika shule za shule za upili katika vipindi tofauti. Hata hiyo utafiti huu unaegea zaidi kwa maudhui makuu ya kazi hizi ,kuyatathimini na na kuyaoanisha na mambo halisi katika jamii katika vipindi hivi vya utahini lengo kuu likiwa kuchunguza uhalisia wa maudhui makuu katika jamii na umuhimu wake kwa wanafunzi katika vipindi vile. Utafiti huu una sehemu tatu: sura ya kwanza inahusisha : suala la utafiti , maswali ya utafiti,malengo ya utafiti, mihili ya nadharia, sababu za kuchagua mada , upeo na mipaka na uteuzi wa data na uwasilishaji hata. Sura ya pili itashughulikia historia fupi ya waandishi wa tamthilia za Mstahiki Meya (2009)na kigogo(2016), udurusu wa maandishi ya watafiti wengine ili kupata maoni yao kuujenga utafiti huu.Sura ya tatu itahusiana na mbinu za utafiti pamoja na zile za uchanganuzi wa data. Katika kukusanya data, utafiti huu utatumia mbinu ya kusoma makala maktabani na kusakura katika mitandao.sura ya nne ni sehemu ya uchanganuzi wa data iliyokusanywa kutoka kwa tamthilia teule na majibu ya hojaji za walimu na wanafunzi.sura ya tano ni ya muhutasari wa matokeo, hitimisho na mapendekezo. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.title Utathimini wa maudhui katika tamthilia zilizoteuliwa kutahiniwa katika shule za upili nchini Kenya: Mstahiki Meya (2009) na Kigogo (2016). en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search Dspace


Browse

My Account