Please use this identifier to cite or link to this item:
https://repository.seku.ac.ke/handle/123456789/8048| Title: | Utohoaji na matumizi ya maneno changamani katika lugha ya kiswahili: mifano ya mkanganyiko wa maana na matumizi ya neno “bongofleva” nchini Tanzania |
| Authors: | Lupogo, Issaya |
| Keywords: | Utohoaji Maneno Changamani Mkanganyiko Bongofleva |
| Issue Date: | 2024 |
| Publisher: | South Eastern Kenya University |
| Citation: | Dira ya lugha, Juzuu 1, Na. 1, 81-92, 2024 |
| Abstract: | Lugha ya Kiswahili kama zilivyo lugha zingine ina kawaida ya kutohoa maneno kutoka lugha mbalimbali. Miongoni mwa maneno yanayotoholewa ni maneno changamani, yaani neno moja linaloundwa na maneno zaidi ya moja; mfano, neno Bongofleva (lililotokana na kirai cha Kiingereza Bongo Flavour). Kumekuwa na mkanganyiko wa mawazo kuhusu maana ya Bongofleva na mwasisi wa neno hilo. Makala hii inaonesha mawazo mbalimbali yanayokinzana kuhusu masuala hayo mawili. Makala hii ni matokeo ya mapitio ya maandiko na tajiriba ya mwandishi katika uga wa muziki wa Bongofleva akiwa mdau, mfuatilitiaji, mchambuzi na msanii wa muziki huo. Aidha, sehemu ya data zilishadidiwa kwa kufanya mahojiano na msanii na mtangazaji wa zamani aitwaye KCB. Makala hii imebaini kwamba jina “Bongofleva” liliasisiwa na kutumiwa kwa mara ya kwanza na Mhagama Pesambili (aliyewahi kuwa mtangazaji wa Radio One) na KCB katika kipindi cha DJ Show. Kuhusu maana ya Bongofleva, makala inapendekeza kwamba aina zote za miziki zinazopatikana nchini Tanzania zipo chini ya mwamvuli (kapu) wa Bongofleva kwa kujikita katika mantiki kwamba Bongofleva ni neno lililotoholewa kutoka katika lugha ya Kiingereza “Bongo Flavour” likiwa na maana ya msingi ambayo ni ladha kutoka Bongo/Dar/Tanzania. |
| URI: | https://jadilu.seku.ac.ke/index.php/jadilu/article/view/26/32 http://repository.seku.ac.ke/xmlui/handle/123456789/8048 |
| ISSN: | 3079-3882 |
| Appears in Collections: | School of Humanities and Social Sciences (JA) |
Files in This Item:
| File | Description | Size | Format | |
|---|---|---|---|---|
| Lupogo_Utohoaji na matumizi ya maneno changamani katika lugha ya kiswahili....pdf | abstract | 99.6 kB | Adobe PDF | View/Open |
Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.