Please use this identifier to cite or link to this item: https://repository.seku.ac.ke/handle/123456789/8037
Title: Usambamba wa kisemantiki kati ya methali za kikuyu na za Kiswahili
Authors: Chomba, Esther N.
Keywords: Methali
Usambamba
Kisemantiki
Taswira
Nadharia ya Uelemea Kike
Mkabala wa Ufeministi Hakiki
Issue Date: 2024
Publisher: South Eastern Kenya University
Citation: Dira ya Lugha, Juzuu 1, Na. 1, 93-105 2024
Abstract: Makala hii imeshughulikia usambamba wa kisemantiki kati ya methali za Kikuyu na za Kiswahili kwa kuangazia methali zinazobainisha nafasi ya mwanamke, ndoa na malezi katika jamii hizi. Lengo kuu lilikuwa kuchanganua methali zilizoteuliwa kimakusudi ili kubainisha usambamba wa kimaana unaodhihirika na mtazamo wa wanajamii hawa kuhusu mahusiano ya kimapenzi, ndoa na malezi. Methali nane zimeteuliwa kwa kutumia mbinu kusudio, zikatafsiriwa kwa kutumia tafsiri mawasiliano na kisha kuchanganuliwa kithamano. Ushabihiano wa kimaana wa methali hizi uliangaziwa ili kutimiza madhumuni ya utafiti. Mkabala wa Ufeministi Hakiki wa nadharia ya Uelemea Kike umetumiwa kama kiunzi cha kuchanganulia methali hizi. Makala hii inakusudiwa kutoa mchango adhimu katika nyanja ya fasihi kwa kupanua mawanda ya maandishi yanayohusu methali za Kikikuyu, Aidha, makala hii pia inatarajiwa kuwa kichocheo kwa watafiti ambao wangependa kutalii nyanja zingine za Fasihi Simulizi mbali na kumulika methali kama mojawapo ya vipengele vya utamaduni. Uchanganuzi wa usambamba wa methali hizi umesaidia kubainisha kama jamii hizi zinamkweza au kumkwaza mwanamke. Utafiti huu umebainisha jinsi mwanamke alivyochorwa kitaswira.
URI: https://jadilu.seku.ac.ke/index.php/jadilu/article/view/25/31
http://repository.seku.ac.ke/xmlui/handle/123456789/8037
ISSN: 3079-3882
Appears in Collections:School of Humanities and Social Sciences (JA)

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Chomba_Usambamba wa kisemantiki kati ya methali za kikuyu na za Kiswahili.pdfabstract3.72 kBAdobe PDFView/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.