Please use this identifier to cite or link to this item: https://repository.seku.ac.ke/handle/123456789/8036
Title: Ujitokezaji wa nomino za Kiswahili zinazoibua maana za kitashibiha katika riwaya ya zawadi ya ushindina watoto wa maman’tilie
Authors: Yobu, Judith
Mturo, Neema
Ngesu, Sarah N.
Keywords: Maana
Tashibiha
Nomino Wazi
Nomino Fiche
Issue Date: 2024
Publisher: South Eastern Kenya University
Citation: Dira ya Lugha, Juzuu 1, Na. 1, 128-138, 2024
Abstract: Makala hii imechunguza ujitokezaji wa nomino za Kiswahili zinazoibua maana za kitashibiha katika riwaya ya Zawadi ya Ushindi na Watoto wa Maman’tilie. Data zilipatikana kwa uchanganuzi matini maktabani kwa usomaji makini wa riwaya teule. Matokeo ya utafii yaliyozaa makala hii yameonesha kuwa nomino ni kijenzi muhimu katika muundo wa kuibua maana ya kitashibiha. Pia, yameonesha kuna nomino za wazi na nomino fiche kwenye kazi za kifasihi zinazoibua maana za kitashibiha. Nomino hizi hutumiwa kwa lengo la kuonesha ubunifu na upekee wa kifasihi ambao wasanii hulinganisha hali za maumbile na tabia za jamii ili kutoa mafunzo, kupamba lugha na kuufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa jamii iliyolengwa kupitia tashibiha. Nomino fiche za makala hii zimeibua maana za kitashibiha kupitia nafasi, muundo na matumizi ya nomino kulingana na muktadha wa sentensi za Kiswahili. Makala hii inapendekeza kuwa wataalamu wa fasihi wanapaswa kuchunguza suala la maana za kitashibiha kwenye tanzu zote za fasihi ili kubaini darajia za maneno hasa vitenzi vinavyobeba dhima za kifasihi na kisarufi katika kuibua maana za kitashibiha ili kusaidia dhana ya fasihi linganishi.
URI: https://jadilu.seku.ac.ke/index.php/jadilu/article/view/22/28
http://repository.seku.ac.ke/xmlui/handle/123456789/8036
ISSN: 3079-3882
Appears in Collections:School of Humanities and Social Sciences (JA)

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Yobu_Ujitokezaji wa nomino za Kiswahili....pdfabstract95.42 kBAdobe PDFView/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.