Please use this identifier to cite or link to this item:
https://repository.seku.ac.ke/handle/123456789/7237| Title: | Tafsiri kama nyenzo ya kutandawaza utamaduni wa mswahili: mfano wa Siku Jema (1996) na A Good Day (2019) |
| Authors: | Ngesu, Sarah N. Mrikaria, George |
| Issue Date: | 2022 |
| Publisher: | University of Dar es Salaam |
| Citation: | Journal of the Institute of Kiswahili Studies, Juz. 85, Na. 2 |
| Abstract: | Lengo la makala hii ni kujadili mchango wa tafsiri katika kutandawaza utamaduni wa Mswahili kwa kuangazia riwaya ya A Good Day (Walibora, 2019) kama tafsiri ya riwaya ya Siku Njema (Walibora, 1996) iliyotafsiriwa na Dorothy Kweyu na Fortunatus Kawegere. Tafsiri imekuwa nyenzo muhimu ya kusambaza maarifa ambayo kinadharia yanahusu vipengele vya kiutamaduni kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa. Makala hii inaangazia mwamko wa hivi karibuni wa kutafsiri kazi za fasihi kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Kulingana na Kimutai (2016) na Ngesu na wenzake (2019), kumekuwa na mwamko mpya wa kutafsiri kazi za Kiswahili kwenda Kiingereza na lugha nyinginezo, kinyume na ilivyokuwa awali ambapo kazi mbalimbali zilikuwa zikitafsiriwa kwa wingi kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kusoma na kuchambua matini chanzi na matini lengwa. Makala hii ililenga kuangazia vipengele vya kiutamaduni vilivyohawilishwa kutoka utamaduni chanzi na kuingizwa katika utamaduni lengwa katika matini teule. Modeli ya Newmark (2003) kuhusu ubainishaji wa vipengele vya kiutamaduni iliongoza uchanganuzi wa data za makala hii. Aidha, mbinu linganishi ilitumiwa kuchanganua kiulinganishi matini chanzi na matini lengwa. Mkabala wa kitaamuli ulitumiwa katika uwasilishaji wa data katika majedwali. Matokeo yanaonesha kwamba kupitia njia ya tafsiri, vipengele vya kiutamaduni vimehawilishwa kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa. |
| Description: | DOI: http://doi.org/10.56279/jk.v85i1.10 |
| URI: | https://journals.udsm.ac.tz/index.php/kiswahili/article/view/5621 http://repository.seku.ac.ke/handle/123456789/7237 |
| ISSN: | 0856-048X 2546-2229 |
| Appears in Collections: | School of Humanities and Social Sciences (JA) |
Files in This Item:
| File | Description | Size | Format | |
|---|---|---|---|---|
| Ngesu_Tafsiri kama nyenzo ya kutandawaza utamaduni wa mswahili; mfano wa Siku Jema (1996) na A Good Day (2019).pdf | Abstract | 5.12 kB | Adobe PDF | ![]() View/Open |
Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.
