Please use this identifier to cite or link to this item: https://repository.seku.ac.ke/handle/123456789/4917
Full metadata record
DC FieldValueLanguage
dc.contributor.authorNgesu, Sarah N.
dc.date.accessioned2019-09-11T07:29:01Z
dc.date.available2019-09-11T07:29:01Z
dc.date.issued2017-12
dc.identifier.citationMULIKA Journal, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (University of Dar es Salaam)en_US
dc.identifier.urihttp://repository.seku.ac.ke/handle/123456789/4917
dc.description.abstractMawasiliano katika matibabu ni suala zito linalohitaji kushughulikiwa. Mawasiliano katika taaluma ya afya ni muhimu sana kwa kuwa yanaweza kuathiri pakubwa afya ya wanadamu na kuchangia maendeleo au pia kudumaza maendeleo. Kupokelewa na kusambaa kwa simu za kiganjani katika nchi ya Kenya, Afrika na ulimwenguni kote kumechangia maendeleo si haba katika teknolojia ya mawasiliano. Makala haya yanafafanua umuhimu wa kutumia Kiswahili katika ujumbe mfupi wanaosambaziwa wagonjwa wa UKIMWI, Kenya, chini ya mradi wa kimajaribio wa WelTel. Lengo kuu la mwandishi wa makala haya ni kuonesha kuwa wataalamu wa kimatibabu hawawezi kutoa huduma za kiafya kwa njia yenye ufanisi iwapo mawasiliano baina yao na wagonjwa yanakumbwa na vikwazo vya kimawasiliano. Kikwazo kimojawapo kwa mawasiliano hayo na ambacho kina athari kubwa ni lugha inayotumiwa. Jumbe zinazosambaziwa wagonjwa hawa kuhusu vyakula bora, dawa za kudhibiti maambukizi na makali husambazwa kwa lugha ya Kiingereza. Ni jambo la welekea kueleza kwamba lugha inayotumiwa na watu vijijini huwa ni lugha za asili. Aidha, asilimia kubwa ya wananchi wa Kenya wana ujuzi wa Kiswahili ambayo ni lugha ya taifa na rasmi. Isitoshe, Kiswahili ni lugha ya kibantu zao la jamii ya kiafrika na ni sehemu muhimu ya utamaduni wa kiafrika. Maneno/ Dhana muhimu: Kiswahili, Kenya, teknolojia, ujumbe mfupi, mawasiliano ya kijamii, simu ya kiganjani, huduma za afya.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.subjectKiswahilien_US
dc.subjectKenyaen_US
dc.subjectteknolojiaen_US
dc.subjectujumbe mfupien_US
dc.subjectmawasiliano ya kijamiien_US
dc.subjectsimu ya kiganjanien_US
dc.subjecthuduma za afyaen_US
dc.titleNafasi ya Kiswahili katika Mawasiliano ya Kijamii: Uchanganuzi wa Ujumbe Mfupi Unaosambazwa kwa Wagonjwa wa UKIMWI nchini Kenyaen_US
dc.typeArticleen_US
Appears in Collections:School of Humanities and Social Sciences (JA)

Files in This Item:
File Description SizeFormat 
Ngesu_Nafasi ya Kiswahili katika mawasiliano ya kijamii.pdfAbstract5.45 kBAdobe PDFThumbnail
View/Open


Items in DSpace are protected by copyright, with all rights reserved, unless otherwise indicated.