Tathmini ya nyimbo za kiswahili kama nyenzo ya ufundishaji katika shule za chekechea

Show simple item record

dc.contributor.author Mwanza, Pius M.
dc.contributor.author Ngesu, Sarah N.
dc.contributor.author Musyoka, F. M.
dc.date.accessioned 2025-08-18T16:17:44Z
dc.date.available 2025-08-18T16:17:44Z
dc.date.issued 2025-08-04
dc.identifier.citation European Journal of Linguistics, volume 4, issue 2, 2025. en_US
dc.identifier.issn 2957-4641
dc.identifier.uri https://carijournals.org/journals/index.php/ejl/article/view/3084/3464
dc.identifier.uri http://repository.seku.ac.ke/xmlui/handle/123456789/8132
dc.description.abstract Lengo la Utafiti:Utafiti huu ulinuia kutathmini nyimbo za Kiswahili zinazotumika katika shule za chekechea kama nyenzo ya ufundishaji katika kata nne za Kaunti ya Makueni ambazo ni Mukaa, Kilungu, Kathonzweni na Makueni. Madhumuni ya utafiti huu ilikuwa ni;Mosi, kuainisha aina za nyimbo za Kiswahili zilizotumika kama nyenzo ya ufundishaji katika shule za chekechea nchini Kenya.Pili, kubainisha namna nyimbo za Kiswahili zilivyotumika kama nyenzo ya ufundishaji.Tatu, kufafanua athari za matumizi ya nyimbo za Kiswahili kama nyenzo ya ufundishaji katika shule za chekechea. Mbinu za Utafiti:Kaunti ya Makueni ina idadi ya kata tisa kwa ujumla. Kata hizi nne ziliteuliwa kwa sababu utafiti waawali ulionyesha kwamba kwenye kata hizo kuna shule za chekechea ambazo zina mchanganyiko wa walimu na wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali nchini Kenya na waliozungumza lugha asili tofauti.Shule saba za kiserikali na tatu za kibinafsi ambazo zenye wanafunzi wengi zilishughulikiwa katika utafiti huu. Shule mbili hadi tatu zilichaguliwa katika kila kata kulingana na idadi ya wanafunzi na maeneo ya shule hizo.Mbinu ya kusudio ilitumika kuchagua nyimbo za Kiswahili ishirini na tano kwa jumla. Sampuli lengwa ilikuwa ni shule saba za kiserikali na tatu za kibinafsi. Pia, mbinu ya hojaji ilitumika katika ukusanyaji wa data kutoka kwa walimu.Data ya utafiti huu ilichanganuliwa kwa kutumia njia ya kimaelezo na kitakwimu.Utafiti uliongozwa na nadharia ya kiutambuzi iliyoasisiwa na Jean Piaget mwaka wa 1954. Matokeo ya Utafiti: Utafiti huu umebaini kwamba nyimbo za Kiswahili ni mojawapo ya nyenzo muhimu ya ufundishaji katika shule za chekechea nchini Kenya. Mchango wa Kipekee kwa Nadharia, Sera na Mazoezi: Kwa Nadharia:Utafiti uliongozwa na nadharia ya kiutambuzi iliyoasisiwa na Jean Piaget mwaka wa 1954.Kwa Sera:Nyimbo za Kiswahili zilitumika katika ufundishaji katika sehemu kubwa kwa kuwa zilieleweka na wanafunzi wote.Kwa Mazoezi:Nyimbo za Kiswahili zinazotumika katika shule za chekechea kama nyenzo ya ufundishaji. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher European Journal of Linguistics en_US
dc.subject Nyimbo za Kiswahili, en_US
dc.subject yenzo za Ufundishaji, en_US
dc.subject Shule za Chekechea en_US
dc.title Tathmini ya nyimbo za kiswahili kama nyenzo ya ufundishaji katika shule za chekechea en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search Dspace


Browse

My Account