Abstract:
Lengo la Utafiti:Utafiti huu ulinuia kutathmini nyimbo za Kiswahili zinazotumika katika shule za  chekechea  kama  nyenzo  ya  ufundishaji  katika  kata  nne  za  Kaunti  ya  Makueni  ambazo  ni Mukaa,   Kilungu,   Kathonzweni   na   Makueni.   Madhumuni   ya   utafiti   huu   ilikuwa   ni;Mosi, kuainisha aina za nyimbo za Kiswahili zilizotumika kama nyenzo ya ufundishaji katika shule za chekechea  nchini  Kenya.Pili,  kubainisha  namna  nyimbo  za  Kiswahili  zilivyotumika kama nyenzo ya ufundishaji.Tatu, kufafanua athari za matumizi ya nyimbo za Kiswahili kama nyenzo ya ufundishaji katika shule za chekechea.
Mbinu za Utafiti:Kaunti ya Makueni ina idadi ya kata tisa kwa ujumla. Kata hizi nne ziliteuliwa kwa  sababu  utafiti  waawali  ulionyesha  kwamba  kwenye  kata  hizo  kuna  shule  za  chekechea ambazo zina mchanganyiko wa  walimu na wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali nchini Kenya na waliozungumza lugha asili tofauti.Shule saba za kiserikali na tatu za kibinafsi ambazo zenye wanafunzi  wengi  zilishughulikiwa  katika  utafiti  huu.  Shule  mbili  hadi  tatu  zilichaguliwa  katika kila kata kulingana na idadi ya wanafunzi na maeneo  ya shule hizo.Mbinu ya kusudio ilitumika kuchagua nyimbo za Kiswahili ishirini na tano kwa jumla. Sampuli lengwa ilikuwa ni shule saba za kiserikali na tatu za kibinafsi. Pia, mbinu ya hojaji ilitumika katika ukusanyaji wa data kutoka kwa   walimu.Data   ya   utafiti   huu   ilichanganuliwa   kwa   kutumia njia   ya   kimaelezo   na kitakwimu.Utafiti uliongozwa na nadharia ya kiutambuzi iliyoasisiwa na Jean Piaget mwaka wa 1954.
Matokeo ya Utafiti: Utafiti huu umebaini kwamba nyimbo za Kiswahili ni mojawapo ya nyenzo muhimu ya ufundishaji katika shule za chekechea nchini Kenya.
Mchango  wa  Kipekee  kwa  Nadharia, Sera  na  Mazoezi: Kwa  Nadharia:Utafiti  uliongozwa  na nadharia  ya  kiutambuzi  iliyoasisiwa  na  Jean  Piaget  mwaka  wa  1954.Kwa  Sera:Nyimbo  za Kiswahili   zilitumika   katika   ufundishaji   katika   sehemu   kubwa   kwa   kuwa   zilieleweka   na wanafunzi  wote.Kwa  Mazoezi:Nyimbo  za  Kiswahili  zinazotumika  katika  shule  za  chekechea kama nyenzo ya ufundishaji.