Harakati za Ujitambuaji wa Mwafrika katika Tamthiliya ya Kiswahili

Show simple item record

dc.contributor.author Muusya, Justus K.
dc.contributor.author Kandagor, Mosol
dc.date.accessioned 2025-05-16T07:26:52Z
dc.date.available 2025-05-16T07:26:52Z
dc.date.issued 2024
dc.identifier.citation Dira ya lugha, juzuu 1, na. 1, 139-149, 2024 en_US
dc.identifier.issn 3079-3882
dc.identifier.uri https://jadilu.seku.ac.ke/index.php/jadilu/article/view/21/27
dc.identifier.uri http://repository.seku.ac.ke/xmlui/handle/123456789/8056
dc.description.abstract Tamthilia ya Kiswahili ina historia fupi ikilinganishwa na tanzu zingine, hasa ushairi. Tamthilia za kwanza kuwahi kutafsiriwa kwa Kiswahili na zilizoandikwa kwa lugha hii zilizingatia sana maudhui ya kidini, kizalendo, utetezi dhidi ya dhuluma za tawala za kigeni na hasa ukoloni mamboleo. Kinyume na hali hiyo, tamthilia ya Kiswahili katika kipindi cha kuanzia 1950 hadi miaka ya 2020 imesheheni wingi wa tungo zinazosifia Uafrika na heshima ya mtu mweusi hapa barani Afrika na kote ulimwenguni. Uchunguzi wa tamthilia hizi unadhihirisha kujitolea kwa dhati kwa watunzi wake kuelezea, kutetea na kuhimiza heshima ya Mwafrika. Maudhui yake yanakiuka yale masuala mapevu ya utaifa, uraia na tawala za mataifa ya Kiafrika. Kwa sababu hii, makala hii imenuia kuchunguza namna suala la heshima na kujitambua kwa Mwafrika limeshughulikiwa katika tamthilia ya kisasa. Ili kufikia lengo hili, makala imechunguza kwa kina namna suala hili limesawiriwa katika tamthilia ya Mashetani Wamerudi (Mohamed 2016). Tamthilia hii iliteuliwa kwa kutumia mbinu kusudio. Hii ni kwa sababu usomi awali ulionyesha kuwa tamthilia hii imetumia misingi ya nadharia ya Ujumi Mweusi. Data yenyewe ilikuwa ya kitaamuli na ilichanganuliwa vilevile kwa njia ya kinathari. Makala yalionyesha namna ambavyo mwandishi ameweka wazi hadhi ya Mwafrika na kudhihirisha kuwa amejitambua na anapaswa kutambuliwa na kuheshimiwa na ulimwengu mzima. Hii ni baada ya Mwafrika kuelewa kwamba watu kutoka mabara mengine sio bora kuliko yeye kama ambavyo watu hawa hutaka ieleweke na Mwafrika. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher South Eastern Kenya University en_US
dc.subject Tamthilia en_US
dc.subject Ujumi Mweusi en_US
dc.subject Uafrika en_US
dc.subject Ukoloni Mamboleo en_US
dc.subject Fasihi ya Kiswahili en_US
dc.title Harakati za Ujitambuaji wa Mwafrika katika Tamthiliya ya Kiswahili en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search Dspace


Browse

My Account