Usawiri wa Miiko ya Jadi katika Jamii ya Sasa: Mifano kutoka Jamii ya Wapare

Show simple item record

dc.contributor.author Sadi, Hatibu
dc.contributor.author Ontieri, James
dc.contributor.author Sengo, Tigiti S.
dc.date.accessioned 2025-05-15T12:32:08Z
dc.date.available 2025-05-15T12:32:08Z
dc.date.issued 2024
dc.identifier.citation Dira ya lugha, juzuu 1, Na. 1, 176-189, 2024 en_US
dc.identifier.issn 3079-3882
dc.identifier.uri https://jadilu.seku.ac.ke/index.php/jadilu/article/view/18/24
dc.identifier.uri http://repository.seku.ac.ke/xmlui/handle/123456789/8053
dc.description.abstract Miiko ni sehemu muhimu inayotoa mwelekeo wa mienendo inayokubalika katika jamii yoyote ulimwenguni. Makala haya yanajadili usawiri wa miiko ya jadi katika jamii ya sasa na mifano ikiwa ni kutoka kwa Wapare wa Mwanga Mkoani Kilimanjaro. Lengo kuu la makala haya ni kubainisha namna miiko ya jadi inavyohusiana na kuakisi moja kwa moja maisha ya jamii katika vipengele nuwai vya maisha. Mjadala wa makala haya uliongozwa na swali lililouliza: Miiko kama kipera kimojawapo cha sanaajadiiya inasawiri vipi maisha ya kila siku ya jamii? Mkabala uliotumika kwenye makala haya ni wa kimaelezo. Mbinu zilizotumika katika utafiti wa makala haya ni mbili. Mbinu ya kwanza ni ya usaili ambayo iliwezesha upatikanaji wa data za awali (msingi) na mbinu ya pili ni ya uchanganuzi wa matini ambayo iliwezesha upatikanaji wa data za upili. Nadharia ya Taalimu Ina Kwao na Fasihi Ina Kwao, ndiyo iliyotumiwa kwenye mwendelezo wa uchunguzi na uchambuzi wa makala haya. Matokeo ya tafiti yalionesha kuwa, miiko ya jadi ni kipera muhimu cha sanaajadiiya kilichofumbata tamathali za semi na hurithishwa kwa njia ya masimulizi. Miiko inasawiri maisha ya jamii na ni mhimili muhimu wa maadili. Miiko hiyo huakisi jamii kitamaduni na kimazingira na hivyo kuendelea kudhihirisha umuhimu usio na shaka. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher South Eastern Kenya University en_US
dc.subject Usawiri en_US
dc.subject Miiko en_US
dc.subject Jadi en_US
dc.subject Jamii ya Sasa en_US
dc.subject Wapare en_US
dc.title Usawiri wa Miiko ya Jadi katika Jamii ya Sasa: Mifano kutoka Jamii ya Wapare en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search Dspace


Browse

My Account