dc.description.abstract |
Makala hii imelenga kubainisha nafasi ya picha katika kukuza upokezi wa msomaji katika vitabu teule vya fasihi ya watoto: Kesho! Kesho! (Hussein, 2009) na Werevu wa Juma (Yahya, 2003). Utafiti huu umechochewa na kuwepo kwa pengo kuhusu jinsi picha hukuza upokezi wa msomaji hususan katika hadithi za Kiswahili teule. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Mwitikio wa Msomaji.Muundo wa utafiti huu umekuwa wa kimaelezo na kitakwimu. Data zilikusanywa kwa kusoma na kuchanganua makala na vitabu teule, pamoja na njia ya mahojiano na wanafunzi wa shule za msingi waliopo ngazi ya gredi ya pili. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa upokezi wa ujumbe huimarishwa ikiwa msomaji atatambua vigezo muhimu katika picha. Vigezo hivi ni kama vile: Mtafitiwa kutambua picha kwenye kitabu polepole ama kwa haraka, kutambua wahusika, rangi na mandhari, kuchanganua ujumbe wa picha kutumia vigezo vya mandhari, ishara, maandishi kwa picha, rangi, nyuso za wahusika na mavazi, upokezi wa ujumbe usiofanana na unaofanana kwenye picha na matini, watafitiwa kufanya masimulizi kulingana na ujumbe walioupokea kutokana na picha kwenye vitabu teule, upokezi kutokana na umilisi, mshikamano na mtiririko wa hadithi, mafunzo ya picha kutokana na upokezi wa ujumbe kwenye picha na matini, kubaini dhima ya picha kulingana na upokezi wa ujumbe katika picha, umakini katika kusoma na kung’amua maandishi na kujadili uhusiano wa picha na maandishi, hali ya nyuso zilizofurahia na zilizo na huzuni kama kigezo cha hisia. |
en_US |