dc.description.abstract |
Makala haya yameonyeshakwambamatumizi ya tafsiri hususanuteuzi wa mikakati ya tafsiri katikaufundishaji wa lugha kama nyenzo ya kurahisisha mawasiliano hukabiliwa na changamoto mbalimbali. Data zilikusanywa kupitia ushuhudiaji na uchambuzi wa nyaraka. Kulingana naCook (2018)tafsiri ni mchakato unaohusisha uteuzi wa mikakati ya tafsiri ambayo ndiyo msingi anaotumia mfasiri anapokabiliwa na tatizolaukosefu wa visawe vya moja kwa moja baina ya lugha chanzi (kuanzia sasa LC) na lugha lengwa (kuanzia sasa, LL). Tafiti tanguliziMohamed (2014),Ngwendu (2016), Ito (2017), Mahi (2018), Navidinia na wenzie (2019), Karimah (2020) na Ngesu (2020) kuhusutafsiri na ufundishaji wa lugha ya kigenihazijachunguza changamoto za uteuzi wa mikakati ya tafsiri katikahali halisi darasaniilazimejiegemeza kuchunguza changamoto za tafsiri kwa jumla. Uteuzi wa mikakati ya tafsiri isiyofaa unaweza kukwamisha mawasiliano katika ufundishaji na unaweza kuwa naathari hasi kwa mwanafunzi anayejifunza lugha. Hivyo, ilionekana ni muhimu kuchunguza uteuzi wa mikakati ya tafsiri katika mchakato halisi wa ufundishaji wa Kiswahilidarasani. Matokeo yanaonesha kwamba walimu na wanafunzi hukabiliana na changamoto mbalimbali kutokana na kutumia mkakati wa tafsirisisisi kwa lengo la kurahisisha mawasiliano. Inapendekezwakuwa walimu ambao hawana maarifa na umahiri katika taaluma ya tafsiri waepuke kutumia tafsiri katika ufundishaji wa Kiswahili. Pia, inapendekezwa kuandaawarsha za mara kwa mara ili kuwasaidia walimu ambao tayari wamesoma kozi mbalimbali za tafsiri ili kuboresha umahiri wao katika tafsiri. Pia, inapendekezwa kuwawezesha walimu na wanafunzi kuwa na vitendeakazi kama vile kamusi thaniya na kamusi wahidiya. |
en_US |