Tafsiri katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni nchini Uganda

Show simple item record

dc.contributor.author Ngesu, Sarah N. M.
dc.date.accessioned 2021-06-21T06:53:15Z
dc.date.available 2021-06-21T06:53:15Z
dc.date.issued 2021-06-21
dc.identifier.uri http://repository.seku.ac.ke/handle/123456789/6271
dc.description Tasnifu ya PhD (Kiswahili), 2021 en_US
dc.description.abstract Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kutathmini matumizi ya tafsiri na mikakati ya tafsiri katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni katika shule za sekondari nchini Uganda. Utafiti ulikuwa na malengo matatu. Mosi, kubainisha mikakati ya tafsiri inayotumika. Pili, kutathmini matumizi ya tafsiri na mikakati ya tafsiri katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili na tatu, kubainisha na kufafanua aina ya changamoto wanazokubana nazo walimu na wanafunzi wanapotumia tafsiri. Katika mchakato wa kutafsiri, mfasiri hukabiliana na tatizo la kupata visawe mbadala baina ya lugha chanzi na lugha lengwa. Ili kukabiliana na tatizo hili, mfasiri hutumia mikakati ya tafsiri. Matumizi ya tafsiri na mikakati ya tafsiri yanaweza kuwa na athari zake katika uhawilishaji wa ujumbe. Mada inayoangaziwa katika utafiti huu inahusu uchangamani wa taaluma mbili ambazo ni tafsiri na ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni. Kwa hivyo, nadharia moja isingeweza kutosheleza mahitaji ya uchanganuzi wa data zilizokusanywa. Utafiti umeongozwa na Modeli ya Vinay na Darbelnet (2004), Nadharia ya Usawe wa Kidhima ya Nida na Taber (2004) na Nadharia ya Umotishaji Lugha ya Dörnyei (1994). Utafiti huu ulichukua mkabala mseto. Mbinu zilizotumiwa kukusanyia data ni pamoja na ushuhudiaji, uchambuzi wa nyaraka na hojaji. Data za utafiti zimewasilishwa kitaamuli na kitakwimu na kwa kutumia majedwali, chati-duara, grafumhimili na michoro. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba walimu na wanafunzi hutumia tafsiri na mikakati ya tafsiri kwa kiwango kikubwa katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili. Pia, matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba walimu hutumia mikakati ya tafsiri ili kukabiliana na tatizo la kutafsiri vipashio vya lugha. Mkakati unaotumiwa mara nyingi katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili ni tafsiri sisisi, ubadilishaji mtazamo, Ubadilishaji kategoria, Usawe na tafsiri-mkopo mtawalia. Pia, imebainika kwamba tafsiri inafaa katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili inapotumiwa pamoja na mbinu nyingine. Kwa kuhitimisha, matokeo yanaonesha kwamba tafsiri inayotumiwa katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili ni ya kimawasiliano ambayo ni tofauti na tafsiri-sarufi iliyotumiwa katika ufundishaji wa Kiyunani na Kilatini. Aidha, matumizi ya tafsiri yana changamoto zake katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili. Inapendekezwa kuratibu mtaala wa ufundishaji wa Kiswahili ili kuwaongoza walimu wa Kiswahili kutumia mikabala mseto ambayo pia itajumuisha tafsiri, badala ya kusisitiza mkabala wa kimawasiliano tu. en_US
dc.description.sponsorship Chuo Kikuu cha Dar es Salaam en_US
dc.language.iso en en_US
dc.title Tafsiri katika ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni nchini Uganda en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search Dspace


Browse

My Account