Usilimisho wa maneno ya mkopo katika lahaja ya Kĩkamba ya Mwingĩ

Show simple item record

dc.contributor.author Ngesu, Sarah N. M.
dc.date.accessioned 2019-09-11T12:56:15Z
dc.date.available 2019-09-11T12:56:15Z
dc.date.issued 2019-09-11
dc.identifier.uri http://repository.seku.ac.ke/handle/123456789/4919
dc.description (Masters of Arts, 2004 en_US
dc.description.abstract Azima ya tasnifu hii ni kufanya uchanganuzi wa kiufafanuzi kuhusu usilimisho wa maneno mkopo katika LAKĨMŨ kwa kutumia msingi wa kinadharia uliochangamano. Kila lugha ni tokeo la mabadiliko, hakuna lugha iliyo ya jinsi moja. Kwa hiyo maneno mkopo huchangia pakubwa mabadiliko haya ya lugha. Kiswahili ni lugha ya Afrika Mashariki na kati ambayo imekua na kujulikana na wengi zaidi kuliko lugha nyingine ya Afrika. Vile vile Kiswahili ni lugha ya Kitaifa, Kibiashara na ya ki+mawasiliano nchini Kenya. Lugha hii imeingiliana na lugha zingine kwa karne nyingi hali ambayo imesababisha Kiswahili kuwa na utajiri wa msamiati kuliko lugha zingine za Kibantu. Tumeibawibu kazi hii katika sura tano. Sura ya kwanza inatoa maelezo ya kimsingi kuhusu ukopaji wa maneno pamoja na usuli wa utafiti. Mambo yanayojadiliwa katika usuli huo wa utafiti ni: mada ya utafiti, lugha na jamii zinazoshughulikiwa, madhumuni ya utafiti, upeo na mipaka ya tasnifu na udurusu wa maandishi. Pia katika sura hii, tumefafanua sababu zetu za kuichagua mada hii, msingi wa kinadharia uliotuongoza na vile vile njia za kufanyia utafiti. Sura ya pili imeshughulikia ulinganishi wa kifonolojia na kimofolojia wa lugha tatu zinazomulikwa katika mtalaa huu. Mambo muhimu katika sura hii yanahusu vibadala vya konsonanti na vile vile miundo ya silabi katika usilimisho wa maneno ya mkopo. Katika sura ya tatu, tumezijadili sababu za kiisimu jamii zilizochangia ukopaji wa maneno katika LAKĨMŨ. Sura hii inaipa kazi hii haiba na kuitofautisha na kazi za awali zilizochunguza maneno ya mkopo. Kwenye sura ya nne, uchanganuzi wa usilimisho wa maneno ya mkopo umefafanuliwa. Tumebambanua sheria zinazowakilisha mabadiliko ya kifonolojia katika usilimisho wa maneno mkopo. Sura ya tano inahitimisha utafiti wetu. Kwenye sura hii, tumetoa muhtasari wa sura zote pamoja na kujadili kauli muhimu zilizozuka wakati wa utafiti. Fauka ya hayo tumefasili umuhimu wa tasnifu na kutoa mapendekezo kuhusu vipengele vya kufanyiwa utafiti. en_US
dc.description.sponsorship University of Nairobi en_US
dc.language.iso other en_US
dc.title Usilimisho wa maneno ya mkopo katika lahaja ya Kĩkamba ya Mwingĩ en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search Dspace


Browse

My Account