Tathimini ya maudhui katika tamthilia teule za kiswahili zinazotahiniwa shuleni za upili nchini Kenya: Mstahiki Meya (2009) na Kigogo (2016).

Show simple item record

dc.contributor.advisor Chomba, Esther N.
dc.contributor.advisor Mwangangi, Franscisca M.
dc.contributor.author Muthui, Evelyn Kakivi
dc.date.accessioned 2019-07-17T07:00:42Z
dc.date.available 2019-07-17T07:00:42Z
dc.date.issued 2019-07-17
dc.identifier.uri http://repository.seku.ac.ke/handle/123456789/4495
dc.description.abstract Utafiti huu uliongozwa na lengo la kutathimini maudhui kwenye tamthilia tahininiwa za karne ya ishirini na moja na kuyalinganisha na matukio halisi katika jamii.Mtafiti pia alitakikana kubaini ufaafu na uhalisi wa maudhui ya tamthilia tahiniwa za karne ya ishirini: tamthilia za Mstahiki Meya (Arege, 2009) na Kigogo (Kea, 2016). Tatizo kuu la utafitihuu lilikuwa kuwepo kwa ukuruba wa maudhui katika kazi za waandishi tofauti kwa nyakati tofauti na hata jinsia tofauti. Kuteuliwa kwa kazi za tamthilia zenye maudhui sawa katika vipindi tofauti vya utahini piakulichochea mtafiti kutaka kubaini ufaafu wa tamthilia tahiniwa.Utafiti uliongozwa na maswali yafuaatayo: ni maudhui yapi makuu yanayojitokeza katika tamthilia za Mstahiki Meya (Arege, 2009) na Kigogo. (Kea, 2016)?Ni masuala yapi makuu ya kijamii yaliyosheheni katika kipindi cha kuidhinishwa kutahiniwa kwa tamthilia hizi?Je, kuna ulinganifu wa uhalisi wa maudhui ya kazi hizi na uhalisi wa kijamii?Utafiti huu ulitegemea zaidi data iliyokusanywa kutoka kwa usomaji wa maktabani na hojaji kwa walimu na wanafunzi katika shule za upili kwenye kata ndogo ya Nzambani kaunti ya Kitui. Mtafiti pia alisoma na kubaini maudhui kaitka tamthilia teule. Baada ya kusoma, mtafiti aliyaandika maudhui yale kama data ya utafiti akitoa mifano mwafaka ili kusisitiza ukweli kuwa maudhui ya waandishi tofauti na nyakati tofauti ni sawa. Uchanganuzi wa madhui kwenye tamthilia ulikuwa wa kimaelezo tu kuonyesha ukuruba na uhalisi wa maudhui.Ilikupata maudhui ya kijamii, mtafiti alikusanya data kutoka kwa vyombo vya habari kama vile magazeti, kusoma majarida na ripoti mbali mbali. Mtafiti pia alipata data jumuishi kutoka kwa hojaji za walimu na wanafunzi wa kidato cha tatu na nne ili kuwa kiwakilishi cha jamii. Data hiyo iliwasilishwa katika jedwali kupata idadi ya waliotoa jibu la ndio au la kutegemea swali. Idadi ya waliojibu ndio au la zaidi iliwasilishwa katika mchoro wa kisayansi kwa kutumia mbinu ya OriginProili kupata picha kamili.Matokeo ya utafiti yalikuwa kwamba tamthilia zinaendeleza maudhui makuu sawa na yaliyo wazi katika jamii. Ilibainika wazi kuwa maudhui ya tamthilia yanaifaa jamii kwa kuendeleza elimu na maadili kwa mujibu wa mtaala wa elimu. Tafiti zaidi zinaweza kufanywa kwa tanzu zingine za fasihi andishi kama vile kulinganisha maudhui katika riwaya na hadithi fupi, au pia kutumia nadharia zingine kama vile uhalisia wa kijamaa ili kuchunguza naudhui na vigezo vingine vya uteuzi wa tamthilia. en_US
dc.description.sponsorship South Eastern Kenya University en_US
dc.language.iso en en_US
dc.title Tathimini ya maudhui katika tamthilia teule za kiswahili zinazotahiniwa shuleni za upili nchini Kenya: Mstahiki Meya (2009) na Kigogo (2016). en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search Dspace


Browse

My Account