Mielekeo ya wanafunzi wa shule za upili kuhusu methali kinzani; uchunguzi katika kata ya Kitui mjini; kaunti ya Kitui; Kenya

Show simple item record

dc.contributor.author Mbusya, Catherine M.
dc.date.accessioned 2019-06-07T07:43:04Z
dc.date.available 2019-06-07T07:43:04Z
dc.date.issued 2019-06-07
dc.identifier.uri http://repository.seku.ac.ke/handle/123456789/4461
dc.description Shahada ya Uzamili, 2019 en_US
dc.description.abstract Utafiti huu unahusu kuchunguza mielekeo ya watumiaji lugha ya Kiswahili kuhusiana na ukinzani katika methali. Kwa mfano methali, Fuata nyuki ule asali na Fuata nyuki ufe mzingani. Utafiti huu umeongozwa na nadharia mbili; nadharia ya mguso na nadharia ya umaanishaji. Katika upande wa ukusanyaji data, utafiti huu ulitumia hojaji kwenda nyanjani na udurusu wa kina kuhusu methali za Kiswahili. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kubaini na kuchanganua mielekeo ya wanafunzi na walimu wa fasihi ya kiswahili kuhusu kuwepo na methali ambazo maana zake zinakinzana. Matokeo yalibaini kwamba idadi kubwa ya watafitiwa ina mwelekeo chanya kuhusiana na suala lililotafitiwa. Baadhi ya sababu zilizochangia watafitiwa kuwa na mwelekeo chanya ni pamoja na maoni kwamba methali hizi zilizo na maana kinyume humsaidia mwanajamii kutafakari kabla ya kuchukua mwelekeo fulani na labda kuepuka matatizo ya baadaye. Mojawapo ya majukumu ya methali ni kushauri. Hivyo basi, ukinzani utakupa nafasi ya kuchagua ushauri unaokufaa binafsi na upi wa kutupilia mbali. Aidha, kila methali huwakilisha hali halisi ya maisha. Maisha yenyewe yamejaa hali kinzani kama vile urafiki/uadui, wema/ubaya, furaha/huzuni na kadhalika. Kwa kuzingatia kauli hii, kila methali huwakilisha hali fulani. Kwa mujibu wa baadhi ya waliotafitiwa, ukinzani huleta mwelekeo hasi. Walitetea kauli hii kwa kusema kuwa methali zinapokinzana huzua utata na hali ya kumchanganya mtumiaji lugha asijue methali gani itamfaa kwani moja inakuongoza huku, nayo nyingine inakutuma kule! Utafiti huu ulibaini kuwa walimu wana changamoto kubwa sana wanapoelezea maana na matumizi ya methali zinazobishana kwa wanafunzi wao. Asilimia mia moja ya walimu wa fasihi waliotafitiwa walitoa changamoto wanazokumbana nazo wanaposomesha suala la ukinzani katika methali za Kiswahili. Ubishi upo katika methali za Kiswahili lakini iwapo kila methali itatumika katika muktadha, hali na kwa hadhira mwafaka suala la ubishi huu halitakuwa changamoto kubwa. Jambo la msingi litakalozingatiwa ni maana (ufaafu) na matumizi ya methali mahususi. Nadharia ya umaanishaji inashikilia kuwa fasihi inapaswa kuwa na maana. Maana itapatikana baada ya kutumia kila methali katika muktadha na mazingira mwafaka, ndiposa mguso au athari ya fasihi ipatikane (ili fasihi iweze kutekeleza jukumu lake katika jamii). en_US
dc.language.iso en en_US
dc.title Mielekeo ya wanafunzi wa shule za upili kuhusu methali kinzani; uchunguzi katika kata ya Kitui mjini; kaunti ya Kitui; Kenya en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search Dspace


Browse

My Account